Headline:-

+25577686242
info@aeqsmz.go.tz | FAQs
Revolution Government Of Zanzibar
Ministry Of Infrastructure, Communication & Transport
Architects, Engineers & Quantity, Surveyors Registration Board
Latest News
AEQSRB wafanya ziara Dar na Dodoma 29-Aug, 2025 09:03:32
Bodi ya Usajili Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji Majengo Zanzibar pamoja na watendaji waefanya Ziara ya siku tatu kuanzia tarehe 20/08/2025 hadi tarehe 23/08/2025 jijini Dar es Salaam na Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi wajumbe,na watendaji walipata fursa ya kutembelea na kukagua ofisi za Bodi ya Usajili Wahandisi pamoja na kufanya kikao katika ofisi ya (ERB) Dar es Salaam kwaajili ya kufanya mapitio ya makubaliano yaliyofanywa mwezi Novemba 21/2023 Jijini Mwanza.

Lengo la ziara hiyo ni utekelezaji wa makubaliano ya Ushirikiano baina ya Bodi ya Usajili Wahandisi Zanzibar (AEQSRB), Bodi ya Usajili Wahandisi Tanzania (ERB) na Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Tanzania (AQRB) kwa kufanya vikao katika ofisi zao zilizopo Dodoma.

Mwenyekit wa bodi Yasser de costa amesema ziara hiyo yenye lengo la mashirikiano ni muhumu kwa kubadilishana uzoefu pamoja na kushauriana mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Ujenzi.

Nae Mrajis wa Bodi Mhandisi Mansour Rashidi amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kukaa pamoja katika marekebisho ya sheria yanayoikabili bodi ya wahandisi zanzibar ili wataalamu wanaosajiliwa kwa Upande wa Zanzibar waweze kutambuliwa na upande wa Tanzania bara.

Ziara hiyo ilianzia katika Ofisi za Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) Dar es Salaam, bodi ya Usajili Wabunifu Majengo (AQRB) Na Kuhitimishwa katika Bodi ya Usajili Wahandisi Jijini Dodoma.